DARASA LA ALHAMIS na DR. CHRIS MAUKI: TABIA ZA WATU WALIOFANIKIWA AU WENYE MAZINGIRA YA KUJA KUFANIKIWA

Chriss.jpg

 

Kufanikiwa ni kiu ya kila mmoja ingawa ukweli ni kwamba wengi wetu tunabaki tunayatamani mafanikio wakati hatuna mazingira yeyote ya kuruhusu mafanikio hayo yawepo au yatujie. Hapa nakuletea tabia za watu wawili tofauti, mmoja akiwa ni mtu mwenye mafanikio au yule ambaye ana mazingira ya kuja kufanikiwa na mwingine ni mtu asiye na mafanikio na asiye na mazingira ya kufanikiwa maishani. Nitaanza na tabia za watu wenye mafanikio;

1. Ni watu wenye kushukuru kwa kila jambo, sio wenye kutoa lawama
2. Ni watu wenye tabia ya kupongeza pale wanapoona mwingine anastahili pongezi
3. Ni watu wenye tabia ya kusamehe, tena wanasamehe kwa urahisi wala sio kwa kuombwa na kulazimishwa
4. Ni watu wasioona uchungu kuwapongeza wengine au kukubali wengine wanapopata ushindi wa aina yeyote, na sio tu kuwapongeza bali pia hawaoni ugumu kuwasaidia au kuwashauri wengine ili wafanikiwe zaidi
5. Ni watu wanaokubali wakati wote kubeba majukumu au lawama pale wanaposhindwa kufanya inavyopaswa, sio wenye kujitetea au kujaribu kukwepa majukumu
6. Ni watu wenye tabia ya kupenda kusoma kitu kila siku, sio wavivu wa kusoma au kutafuta taarifa na ujuzi
7. Ni watu wenye tabia ya kuweka utaratibu wa nini kinafanyila leo na nini kitafanyika kesho na kwa nini kifanyike, sio watu wanaoburuzwa na mazingira yanaowazunguka au kuendeshwa na marafiki zao
8. Sio watu wenye kuzungumza sana kuhusu watu wengine na madhaifu yaw engine bali ni wenye kuzungumza zaidi kuhusu mawazo ya kujenga au mawazo ya kimaendeleo
9. Mara zote wana kiu ya kuona wengine wanafanikiwa, hata kama mafanikio hayo yatayazidi yale wao walionayo
10. Sio wachoyo katika kutoa taarifa au ujumbe wowote muhimu kwa mtu yeyote, maana wao hawana uchungu na mafanikio au ushindi wa mwingine
11. Ni watu wenye kuonyesha furaha wakati wote, sio wenye kununa, kuzira na kuwa na huzuni mara kwa mara
12. Ni watu wanaoweka malengo na kuongozwa na malengo katika maisha yao ya kila siku, sio wanaokurupuka kufanya mambo kwa hisia, misukumo au mashindano tu
13. Sio waoga wa mabadiliko, bali hutamani mabadiliko chanya na yenye kujenga na kuleta maendeleo, na kwahiyo mara zote kuyawezesha mabadiliko kutokea kwao na kwenye maisha ya wengine na sio kuyapinga
14. Kwao kujifunza ni tabia endelevu sio jambo linalotokea wakati wakiwa shuleni tu, wao huhesabu maisha ya kila siku ni kama shule
15. Kiu na msukumo wa maisha yao ya kila siku ni katika kusababisha mabadiliko, aidha mabadiliko kwao wao binafsi au kwa wale wanaowazunguka.

 

UsikoseĀ  part 2 Alhamis ijayo, Tabia za watu wasiofanikiwa au wasio na mafanikio na ambao hawatokuja kufanikiwaDr. Chris Mauki. An expert in Relationships, Social and Counseling Psychology. Lecturer in Psychology: UDSM. Inspirational & Motivational speaker. Family man


4 thoughts on “DARASA LA ALHAMIS na DR. CHRIS MAUKI: TABIA ZA WATU WALIOFANIKIWA AU WENYE MAZINGIRA YA KUJA KUFANIKIWA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *