SESSION DETAILS

Single session

Session ya ushauri kwa mtu mmoja ni sh. 70000/= na couple session (au session ya watu wowote wawili) ni sh. 120000/= Maongezi na ushauri huchukua dakika 45 hadi 60 (lisaa limoja). Ushauri katika kundi, watu zaidi ya wawili kwa wakati mmoja (group counseling) hii huchukua muda mrefu zaidi na gharama yake ni sh. 250,000/= kwa session moja. Ofisi ipo ESAURP VILLAGE Survey, “University road” njia ya kuelekea chuo kikuu cha Dar es Salaam, au Makongo, au chuo cha ardhi, baada tu ya kumaliza geti la mlimani city, mkono wa kulia utaona maandishi kwenye bango kubwa jeupe “ESAURP VILLAGE”. Booking hufanywa kwa simu siku moja au mbili kabla na malipo hufanywa kabla ya kukutana kwa namba 0713 407182 tigopesa na 0762 247863 mpesa. Idadi ya sessions tutakazokutana hujulikana baada ya uchambuzi wa tatizo katika mkutano wa mara ya kwanza. Malipo ya ushauri yaliyotajwa hapo juu hulipwa kabla ya siku ya kuonana ili kurahisisha mchakato mzima wa kuwekewa muda wako. Kwa mawaasiliano zaidi +255 717 052 328 au +255 713 407 182. au chrismauki57@gmail.com. Kumbuka kwamba muda uliopotea kwa kuchelewa hautofidiwa na session isiyohudhuriwa italipiwa. Karibu sana.

PARENTING SESSIONS (Session kati ya mzazi/wazazi na mtoto/watoto)
Tatizo lolote linaloripotiwa na mzazi kumhusu mtoto, session ya kwanza nitalazimika kuongea na mzazi pekeyake (single session, na gharama yake ni 70000/-) au wakiwa wazazi wawili (couple session) na baada ya hapo ndipo nitaongea na mtoto (another single session, gharama yake ni 120000/-) na baada ya hapo ndio nitaongeaa na mtoto (session nyingine 70000/-). Idadi ya kukutana na mtoto itategemea na yatakayojiri ktk session ya kwanza. Mwishoni ni lazima kuwa na session ya mrejesho (feedback session) kwa mzazi. Kila session katika hizi hujitegemea katika malipo na malipo hufanywa kabla ya kukutana kwa namba 0713 407182 tigopesa na 0762 247863 mpesa. Kumbuka kwamba muda uliopotea kwa kuchelewa hautofidiwa na session isiyohudhuriwa italipiwa. Karibu sana.

BAADA YA KUFANYA BOOKING
Fahamu kwamba, taarifa ya kuahirisha kwa aina yeyote inaweza kutolewa angalau masaa manne kabla ya muda wa kukutana, Muda hautaongezwa endapo mtu atachelewa na kutokufika kwa aina yeyote kutalipiwa kiwango kile kile cha ada ya ushauri. Asante na karibu sana.

KWA USHAURI WA SIMU AU EMAIL (Kwa walioko mbali)
Wale wote wanaolazimika kushauriwa kwa njia ya simu gharama ya session ni ile ile Tsh 70,000/= kwa kila session ya ushauri. Gharama za mawasiliano 10,000/= itaongezwa kwenye kila session ili kuwezesha mawasiliano ya simu, labda kama mteja ndiye anayepiga simu hiyo. Kwa wale wanaotumia email au barua pepe, malipo hufanywa mara moja tu ambayo ni sh 250,000/= na baada ya kufanya malipo, mawasiliano yataanza kwa muda wote wa uchambuzi na utathmini wa tatizo hadi tutakapofikia hitimisho. Pale njia ya skype itakapotumika, gharama inakuwa sh.70000/= kwa session kama ilivyo kwa session za kawaida. Malipo yote hufanywa kabla ya kuonana kwa namba 0713 407182 tigopesa au 0762 247863 mpesa.

HUDUMA NJE YA OFISI
Kama italazimika mimi kumfuata mtu nje ya ofisi kwa sababu zozote zile ikiwemo za kiafya au mtu kukosa nafasi ya kutoka huko aliko basi malipo ya ushauri “session fee” ni sh. 150000/= pamoja n ash 30000/= ya usafiri

KARIBU OFISINI

Karibu ofisini (ESAURP VILLAGE: Linda house-ground floor, mlango wa mwisho wenye jina Dr. Chris Mauki), kwa ajili ya ushauri zaidi. Ni karibu kabisa na Mlimani City